Maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani la Kimataifa

Kwa Muungano wa Kongani la Kimataifa, neno ‘maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani za ‘Kimataifa’ humaanisha “maeneo yanayo milikiwa, kusimamiwa na kuhifadhiwa na watu wa asili na jamii za wenyeji wa eneo husika”. [1]

Hii inamaanisha hali ya miaka ya nyuma, ilithibitisha jinsi inayobadilika ambavyo imekuwa na majina mengi tofauti ulimwenguni. Katika mazingira mbalimbali ya kisiasa, zinaweza kujulikana kama ‘mali ya nchi’, mali ya ‘wakereketwa wapenda mazingira’, maeneo ya mababu, maeneo yaliyohifadhiwa ya jamii, maeneo ya kiimani ya asili, maeneo ya baharini na uvuvi yanayosimamiwa na jamii, na mengine mengi.

Kwa wamiliki wa ‘maeneo ya hifadhi za jadi’ kama haya, uhusiano kati ya jamii na eneo lao ni mkubwa zaidi kuliko jinsi unavyoweza kueleza. Ni mahusiano yao ya kipato cha kujikimu, nishati na afya kimazingira. Ni chanzo cha utambulisho na utamaduni, kujitawala na uhuru. Ni kiungo cha muunganiko kati ya vizazi, kuhifadhi kumbukumbu kutoka zamani na kuunganisha kwa siku zijazo wanazozitarajia. Ni msingi ambao jamii hujifunza, kutambua tunu/thamani na kuendeleza mahusiano na kujitawala. Kwa wengi, pia ni uhusiano kati ya ukweli unaoonekana na usioonekana, mali na utajiri wa kidini/itikadi. Katika eneo na asili yapo maisha ya jamii na utu, na kujitawala kama watu.

Maeneo ya hifadhi ya jadi ndiyo msingi wa madhumuni ya Muungano wa Kongani la Kimataifa na Wanachama wake. Kwa kuchukulia mchanganyiko wa sifa zao za kimataifa na uchanganuzi, [2] uliopo, muungano umepitisha namna itakayotumika:

Kongani eneo la hifadhi ya jadi la Kongani la Kimataifa lipo popote:

  • Kuna uhusiano wa karibu na wa kina kati ya eneo na watu wake walio wamiliki wa asili au jamii ya mahali hapo. Uhusiano huu kwa kawaida huambatanishwa na historia, utambulisho wa kijamii, mila na tamaduni, hali ya kiimani/kidini na/au utegemezi wa watu kwenye eneo kwa ustawi wao wa hali na mali. [3]
  • Wamiliki au jamii hufanya na kutekeleza [4] (peke yake au pamoja na watendaji wengine) maamuzi na kanuni kuhusu eneo husika kupitia #taasisi ya utawala inayofanya kazi (ambayo inaweza itambulike au isitambulike na watu wa nje au kisheria katika nchi husika).
  • Maamuzi ya utawala na kanuni [5] (kwa mfano, kuhusu kupata na kutumia ardhi, maji, viumbe hai na zawadi nyingine za asili) [6] na juhudi za usimamizi za watu husika au jamii kwa ujumla huchangia katika #uhifadhi wa maliasili (yaani; uhifadhi, matumizi endelevu na urejesho, kama inavyofaa, wa mifumo ikolojia, makazi, aina ya viumbe na mimea, maliasili, mandhari za nchi kavu na mandhari ya bahari), [7] vilevile kwa vipato vya kujikimu na ustawi wa jamii.

Maeneo ya hifadhi katika muktadha huo na maeneo mbalimbali huonyesha sifa hizi tatu muhimu kwa viwango tofauti. Wamiliki wametilia maanani umuhimu wao, wakitaka yadumishwe na kuimarishwa.

  • Maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani yaliyokamilika— hutimiza sifa hizi tatu, huku
  • Maeneo yalikuwa na hali nzuri ila kutokana na michakato ya kihistoria na misukosuko iliyapata maeneo ya hifadhi ya jadi yalianza kuharibiwa ila bado yanaweza kurudishwa na kuboreshwa.
  • Kongani zinazotarajiwa zina uwezo wa kuendeleza zile sifa tatu, na jamii za wamiliki ziko tayari kufanyia kazi hili.

Maeneo ya hifadhi ya jadi yanahitaji ‘kutambulika’?

Mbali na ‘kukamilika’, ‘kuharibika’ au ‘kutarajiwa’ ni kipengele cha kutambulika kwa maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani. Hili lazima liwe, kwanza kabisa, kujitambua kwa jamii ya wamiliki yenyewe, – la majadiliano ya ndani na kujitambua na kujivunia. [8] Kisha kutambulika kunaweza kufanywa na washirika walio katika ngazi moja, kama vile watu wengine wa asili na jamii za wenyeji, ambao mara nyingi ni muhimu katika kutoa msaada na ushauri. Hatua zaidi zinahusisha kutambuliwa [9] na mamlaka za mitaa, manispaa husika, serikali za mikoa, serikali za kimataifa, [10] mashirika ya kimataifa au wahusika wengine wa kijamii, kama vile mahakama.[11]

Ingawa ni nadra kwamba Kongani inayostawi haijitambui yenyewe, Kongani zinaweza kustawi huku zikitambuliwa kikamilifu, kutambuliwa kwa sehemu, au kutotambuliwa kabisa na wenzao wote, na ngazi mbalimbali za serikali au na watendaji wengine wa nje. Hali ambayo ni mbaya ni wakati maeneo ya hifadhi za jadi — yanatambulika vibaya au isivyofaa

Masijala za Kongani za Kimataifa ni orodha ya maeneo ya hifadhi za jadi yanayotambulika kwa pande zote, ambayo huanzishwa kupitia msaada wa washirika walio katika ngazi moja na michakato ya mapitio, ambayo hutofautiana katika hali na tamaduni mbalimbali. Masijala hii ya kimataifa inayoshikiliwa na Kituo cha Ufuatiliaji wa Uhifadhi Ulimwenguni cha shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira iliyoanzishwa kwa kukusanya seti tofauti za hali za eneo binafsi.[12] Inaboreshwa, na pia itapitiwa, kwa msaada wa washirika walio katika ngazi moja na michakato ya mapitio katika nchi mbalimbali. Maeneo ya hifadhi za jadi pia yameorodheshwa katika kanzidata zisizo maalum, kama vile Kanzidata ya Dunia ya Maeneo yaliyohifadhiwa ambayo pia inasimamiwa na Kituo cha Ufuatiliaji wa Uhifadhi Ulimwenguni.

Zaidi ya kutambuliwa ipasavyo au isivyofaa, maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani—yanaweza kuungwa mkono ipasavyo au isivyofaa. Tena, msaada usiofaa ni sababu ya kutia mashaka. Muungano wa Kongani umezingatia sana kuelewa njia ambazo maeneo ya hifadhi za jadi ya Kongani —#yanavyoweza kutambuliwa na #kuungwa mkono ipasavyo – katika kiini cha dhamira yake ya kisheria na sababu ya kuwepo kwake.

Mifano ya maeneo ya hifadhi za jadi ya Kongani yaliyokamilika, yaliyoharibiwa na yanayotarajiwa

Eneo la Kongani lililokamilika

Eneo la Kongani inayojitambua — Yapú ‘Umu-Kaya Yepa’ Resguardo (mkoa wa Vaupès, Kolombia). [13]

Kolombia inatambua uhuru wa kisiasa na kiutawala wa ardhi ya asili iliyoandaliwa chini ya jina la Resguardos. Watu wa asili wanatambulika kuwa na haki za pamoja a ardhi ambazo haziwezi kunyang’anywa, zisizoweza kutwaliwa na zinazoshikiliwa kwa ajili ya vizazi milele. Haya yote yanahakikisha usalama wa umiliki wa muda mrefu [14]. Aidha, wanapokea fedha ili kuendeleza mifumo yao ya afya na elimu kwa uhuru. Msitu wa kitropiki wa hekta 150,000 wa eneo la hifadhi ya jadi la Yapu kihistoria umekuwa ukitawaliwa na kusimamiwa na viongozi wa kiroho wa mahali hapo (Kumuã), kwa kutumia sheria za kimila kulingana na tunu za kitamaduni (ingawa uanzishwaji wa Resguardo ulianza tu 1982).

Kongani la Yapu si sehemu ya mfumo wa kimataifa wa maeneo yaliyohifadhiwa na hivyo halitalindwa iwapo serikali ya Kolombia itakubali makubaliano ya uchimbaji madini, mafuta na gesi kwenye ardhi yake – ambayo inaweza kuwa na uharibifu mkubwa. Jamii, hata hivyo, inamiliki haki za pamoja za ardhi. Taasisi yake ya kitamaduni inaweza kutangaza na kutekeleza kanuni za kimila na watu wake wana uhuru wa kuishi kulingana na maarifa yao ya jadi, tunu na imani. Haya yote hadi sasa yameruhusu eneo hilo kubaki likiwa limehifadhiwa vizuri huku bioanuwai yake ikitumiwa kwa uendelevu na wamiliki wake.

Kongani zilizoharibiwa

Kongani zilizoharibiwa na ‘maendeleo’— maeneo ya hifadhi ya jadi ya wafugaji wa asili Kusini mwa Ethiopia. [15]

Kwa karne nyingi, jamii za wafugaji na wafugaji-wakulima wa maeneo kame ya Ethiopia zimeishi katika mazingira magumu kwa kutumia kwa uangalifu raslimali kadhaa za ziada kama maji, malisho, misitu, ardhi, na wanyamapori. Kuzifikia rasilimali hizo kulitegemea haki za mtu binafsi na za pamoja za kimila, zikitumika kwa viwango tofauti katika jamii kwa nyakati tofauti, pamoja na mtindo wa maisha wa kuhamahama, mifumo ya kusaidiana na mshikamano wa ndani na katika makundi, na kanuni maalum za kulinda miti na vipengele vya mazingira vingine muhimu.

Maeneo ya jamii za wafugaji yalijumuisha maeneo yenye thamani ya juu ya bioanuwai ambayo yalihifadhiwa vyema kwa karne nyingi, kama vile misitu ya mireteni na maeneo ya visima vya tulaa ya Oromo Borana, tambarare zenye unyevu za Daasanach katika Delta ya Omo, misitu ya ziwa la Kara na ushoroba wa msitu wa Mursi, katika sehemu za juu za Bonde la Omo.

Wakati maeneo ya jamii hizi yalipoingizwa ndani ya nchi ya Ethiopia, mwishoni mwa karne ya 19, mifumo yao ya haki za jamii na utawala na taasisi za kimila haikutambuliwa. Zaidi ya hayo, mipango ya ‘maendeleo’ iliyoanzishwa ilidhoofisha mifumo ya chakula na vipato vya kujikimu ya jumla ya jamii, ambayo ilisababisha uhaba wa chakula.

Leo, jamii bado zinatamani kurejeshwa taasisi zao za utawala na desturi za matumizi ya ardhi [16]. Lakini ujenzi wa bwawa la umeme la Gibe 3 umezuia mafuriko ya mara kwa mara ya Mto Omo, na kukausha maeneo yote ya jamii za kitamaduni za Bonde la Omo la chini. Kana kwamba hiyo haitoshi, sehemu nyingine kubwa za maeneo yao, ikiwa ni pamoja na sehemu zilizokuwa chini ya uhifadhi rasmi katika hifadhi za taifa, zimechukuliwa au kukodishwa kwa kilimo cha umwagiliaji. Kwa hivyo, maeneo ya zamani ya hifadhi za jadi ya Bonde la Omo ya chini hayawezi tena kuendeleza kipato cha kujikimu cha jadi ya jamii.

Kongani iliyoharibiwa inayotafuta kurudi katika hali ya awali

Kongani ambayo ilikuwa na leo haiwezi kuwa kamilifu — Waherero wa Hifadhi ya Ehi-rovipuka, Namibia [17].

Kaskazini mwa Namibia baadhi ya jamii za Waherero zimeanzisha Hifadhi ya Ehi-rovipuka kama eneo ambalo, kulingana na sheria ya Namibia, wanyamapori wanaweza kusimamiwa kwa njia endelevu na jamii. Hifadhi hiyo inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Etosha, mojawapo ya maeneo muhimu yaliyohifadhiwa ya Namibia na ardhi ya mababu wa jamii za Waherero, ambao walifukuzwa kutoka katika ardhi zao karne moja iliyopita. Kwa sasa jamii zinaomba kupata haki fulani za kuzifikia na kuzitumia ardhi za hifadhi na rasilimali ili kuunda upya Kongani lao la awali na kurejesha uadilifu wa desturi zao endelevu za ardhi. Wakati njia ya kutambuliwa ni ndefu, kuwepo kwa Kongani la harakati za maeneo ya hifadhi ya jadi zinaweza kuunga mkono madai yao kwa serikali ya Namibia.

Kutoka Kongani iliyoharibiwa kuelekea kurudi katika hali ya zamani

Marejesho ‘yaliyoboreshwa’ ya Kongani la kimila — Ardhioevu ya Warriparinga, Australia.

Waaborijini wa Kaurna wa Uwanda wa Adelaide wameishi na hisia za kusherehekea mila yao huko Warriparinga, eneo takatifu la asili, kwa maelfu ya miaka. Leo, Warriparinga inajumuisha kilometa za mraba 0.035 za ardhioevu kando ya Mto Sturt (Warriparri) ambayo ni sehemu ya mradi wa urejeshaji. Mpango huo ulianzishwa na ushirikiano kati ya Kaurna na Jiji la Marion, kwa kutumia zana ambazo hupunguza uchafuzi wa mfumo wa mto wa Patawalonga na kurejesha uoto wa asili na wanyamapori. Mradi huo ulifanya kazi sanjari na uanzishwaji wa Kituo cha Utamaduni Hai cha Kaurna, kilichohusika katika uhifadhi na usambazaji wa urithi wa Hadithi za Kuota ndoto za Nchi ya Kaurna kwa vizazi vipya. Kituo hiki kinakuza utalii wa kitamaduni wa asili, elimu na shughuli za mafunzo katika maadili ya upatanisho kati ya jamii za Waaborijini na Wazungu.

Kutoka Kongani iliyoharibiwa hadi iliyorejeshwa hali yake kikamilifu

Mwanzoni mwa milenia mpya, eneo la hifadhi ya jadi la jamii nane za Djola za Manispaa ya Mangagoulack Vijijini (eneo la Casamance, Senegal) lilikuwa limevurugwa kikamilifu. Uvuvi wa kupita kiasi, kuongezeka kwa chumvi kwenye maji na ukataji miti ya mikoko kumechangia uharibifu wa mazingira ya mto, ikiambatana kwa karibu na kuzorota kwa uchumi wa eneo hilo. Bioanuwai ya samaki na upatikanaji wa samaki kwa ujumla ulikuwa umepungua sana. Haya yalifanywa na wavuvi kutoka nje ya eneo hilo walikuwa wakija kwa miaka mingi na injini za boti zenye nguvu na zana za uharibifu zilizomaliza samaki wa eneo hilo.

Jamii za wenyeji zilitaka kurejea kwenye umiliki wao na usimamizi wa kitamaduni wa eneo lao … lakini hawakuwa na njia ya kutekeleza kanuni zozote za uvuvi. Kulingana na maarifa yao na mtazamo wa ulimwengu wa kiimani, walishawishika kuwa wangeweza kurejesha vingi kwenye mfumo wa ikolojia wao na maisha yao… lakini, je, wangeruhusiwa? Kwa kweli, wanafaulu kufanya hivyo, na matumaini yao yakathibitika kuwa yenye haki kabisa.

Mnamo 2009, kwa kujua kwamba Senegal ni Mwanachama wa Mkataba kuhusu Bioanuwai na kwamba Mkataba kuhusu Bioanuwaihuo unahimiza kutambulika kwa ‘maeneo yaliyohifadhiwa ya jamii’, waliweza kuunda upya muundo wao wa utawala na mpango wa usimamizi wa eneo hilo walilolichukulia kuwa “urithi wao utakaohifadhiwa na sisi sote” (kwa lugha ya Djola kapoye wafwolale wata nanang, kwa kifupi Kawawana). Ingawa ustahimilivu na diplomasia, na pia kwa kusisitiza utii wao kwa Sheria ya Ugatuaji ya Senegal, walifanikiwa kupata Kawawana kutambuliwa na Manispaa yao ya Vijijini, Baraza la Mkoa na Gavana wa Casamance [18].

Kufikia 2010, waliweza tena kutekeleza kanuni zao za uvuvi zilizorejeshwa. Na leo mfumo wao wa ikolojia wa mito umejaa tena samaki, chaza na wanyamapori… na kipato chao cha kujikimu na mifumo ya chakula imerejeshwa kikamilifu.

Kutoka Kongani iliyoharibiwa hadi iliyokamilika

Huko Ulaya- eneo la Pori la Jamii la Froxán, Galicia, Uhispania [19].

Jamii ya Froxan ina historia ndefu ya maisha na maendeleo ya kitamaduni katika manispaa ya Galicia ya Lousame, Nordwest Uhispania. Ingawa rasilimali ya pamoja ya jamii inaonyeshwa katika hati za kikabaila za miaka ya 1409, 1527 na 1709, ardhi ilichukuliwa na Serikali katika miaka ya 1930. Mnamo 1977, jamii ilitambuliwa tena rasmi kama wamiliki halali wa Pori la Jamii la hekta 100 la Froxán ambapo walipewa haki za utawala. Eneo hilo hapo awali lilikuwa chini ya uchimbaji madini na kuanzishwa kwa shamba la miti ya kigeni na huduma za misitu za serikali.

Mara baada ya kudhibiti eneo, jamii ya Froxán ilianza shughuli za urejeshaji (kwa mfano, kujaza tena mashimo ya migodi ili kukomesha mtiririko wa tindikali, kurejesha aina ya viumbe vya asili za misitu na makazi, kutokomeza aina ya mimea vamizi na kurejesha mboji ya ardhi ambayo ilikuwa imeharibiwa na maji katika miaka ya 1970) huku ikiendelea na kutumia njia za kitamaduni (kama vile kukusanya kuni, kutumia maji ya chemchemi na kukusanya njugu na uyoga) na shughuli za kitamaduni na kidini (kutumia mimea yenye harufu nzuri ya marashi na mimea ya dawa asili katika Sherehe za majira ya joto

Zaidi ya shughuli za kitamaduni, jamii pia ilijihusisha na shughuli za elimu katika shule zilizo karibu na watu wazima na mashirika yasiyo ya kiserikali, ikihamasisha mamia ya watu. Jamii pia imeshiriki kuandaa sensa ya bioanuwai na mpango wa usimamizi wa urejeshaji wa ardhioevu ambao ulichaguliwa kama mradi wa majaribio ya kimataifa ya kupata uzoefu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Leo, Pori la Jamii la Froxán limeorodheshwa katika Masijala ya Kongani la Kimataifa na Kanzidata ya Dunia ya Maeneo Yanayohifadhiwa.

Kongani inayotarajiwa iliyoibuka kupitia mchakato wa kidemokrasia

Kisiwa muhimu kama makazi ya ndege iliyopitishwa na jamii za wenyeji katika Ziwa Victoria (Uganda) [20].

Kwa muda mrefu visiwa vya Musambwa vimekuwa makazi muhimu ya ndege na maeneo ya mazalia katika Ziwa Victoria. Katika miaka ya hivi karibuni, ukusanyaji wa mayai ya ndege unaofanywa na wavuvi wanaotembelea visiwa hivyo umezidi na kuwa na matokeo hasi ya mazingira. Jamii zinazohusika ziliona tatizo hilo kisha kuwasilisha maazimio kwa Halmashauri za kata zao, na maombi yao yaliunganishwa katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya katika kanuni chache za serikali za mitaa (sheria ndogo) na kutoa amri ya kuanzisha visiwa vya Musambwa kama hifadhi ya ndege. Huu ni mfano wa mpango wa uhifadhi kutoka ngazi ya chini kwenda juu ambao ulitumia vyema taratibu za kidemokrasia na uwezekano wa maamuzi ya ugatuzi yanayojibu matakwa na mahitaji ya jamii za wenyeji. Mpango huo ulipata msaada kutoka mradi wa Mpango wa Ruzuku Ndogondogo wa Taasisi ya Mazingira Duniani lakini msukumo ulikuwa kutoka ndani ya jamii kabisa.

Kuelekea ‘kupatikana’ Kongani?

Kongani katika jangwa la Thar Hindi- Aain Mata Oran. [21]

Jangwa la Thar la India ni mojawapo ya majangwa yenye watu wengi zaidi duniani. Kijijini Sodakore—chenye kaya 236 za wafugaji na wakulima—ni wamiliki wa Aain Mata Oran, wakfu kwa mungu wa Jagdamba/Kumtarai Jogmaya. Orani inatazamwa kama mali ya jamii na eneo takatifu, linalotumiwa kwa malisho lakini kukata miti ni marufuku. Mimea katika Oran, kwa kweli, iko katika hali bora zaidi kuliko katika mazingira ya jirani yake, ambayo kwa bahati mbaya yameharibiwa sana.

Nchini India, kifungu cha sheria cha kutambulika rasmi kwa maeneo yaliyohifadhiwa ya jamii kipo kwenye Sheria ya Haki za Misitu. Mnamo mwaka 2018, Mahakama ya Juu ilitangaza Ora zote kama ‘misitu iliyochukuliwa’, kwa matumaini kuwa itatoa ulinzi dhidi ya shinikizo la uvamizi na uchimbaji madini. Taratibu za utekelezaji wa uamuzi huu, ambazo bado hazijapatikana, zinapaswa kuziweka Orans zote chini ya utawala na usimamizi wa jamii zao za umiliki. Haya ni matumaini makubwa kwa Ain Mata Oran.


Rejea muhimu:

Borrini-Feyerabend na wenzake., 2010 (iliyochapishwa tena 2012); Kothari na wenzake., 2012; Borrini-Feyerabend na Campese, 2017; Farvar na wenzake.

Tazama pia: Tovuti ya Muungano wa Kongani la Kimataifa; Jumuiko la Kongani —Kuhifadhi Maeneo ya hifadhi za jadi – filamu fupi; Maelezo ya Kongani ya uwakilishi kutoka kwa Tovuti ya Kongani; Masijala ya Kongani.


[1]

Kama ilivyoelezwa katika maandishi, neno Kongani la Kimataifa ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza yenye maana ya hifadhi za asili kwa jamii ya asili. Miongo miwili iliyopita, neno hili lilikuwa ‘CCAs’, kifupi pia cha maneno ya Kiingereza yakiwa na maana ya ‘Maeneo Yanayohifadhiwa na Jamii’ (Umoja wa Uhifadhi wa Mazingira Kimataifa, 2004). Ilikamilishwa baadaye na ili kusisitiza jukumu la wamiliki wa asili, ambao pia walionyesha wana ‘maeneo’ badala ya ‘maeneo ya kawaida’ tu. Uundaji wa hivi majuzi zaidi wa ‘maeneo ya hifadhi za jadi’ ulikubaliwa baadaye na wamiliki wengi katika Muungano ili kuelezea tabia pana na ya pande nyingi ya mazingira wanayotunza. Maeneo yaliyohifadhiwa na jamii za asili, yamehifadhiwa kwani mfumo wenyewew umeingia kwenye sera ya kimataifa, na kutoa mwonekano wa jambo hilo.

[2] Hizi ni pamoja na Borrini-Feyerabend na wenzake., 2004a; 2010; Umoja wa Uhifadhi wa Mazingira Kimataifa, 2004; Kothari na wenzake., 2012. 

[3] Uhusiano thabiti unaweza kumaanisha eneo lote au maeneo maalum pekee ndani yake. it.

[4] Ama moja kwa moja au kupitia vyama/mamlaka vilivyo kasmiwa (#Utawala). 

[5] Maamuzi na kanuni zinaweza ziandikwe au zisiandikwe, na wakati mwingine kuunganishwa tu na kile kinachochukuliwa kitamaduni kama tabia inayofaa na inayokubalika.

[6] Katika msamiati huu wote, neno ‘zawadi za asili’ linatumika badala ya ‘maliasili’ kuelezea vipengele vya asili vilivyo hai na visivyo hai ambavyo tunu zake zinatambulika zaidi ya zile za kiuchumi tu.

[7] Muhimu zaidi, uhifadhi hupatikana kutokana na hatua za usimamizi… lakini huenda usionyeshe lengo lililotajwa la wamiliki.

[8] Corntassel anabainisha kuwa kuangazia hasa kujitambua huruhusu jamii kukwepa kuendeleza desturi za kikoloni, ubaguzi wa rangi na mfumo dume zilizopachikwa katika ‘siasa za kutambuliwa’ na mataifa ya walowezi (ona Coulthard, 2014).

[9] Borrini-Feyerabend na wenzake., 2010. Tazama pia #Kutambulika vyema.

[10] Maeneo kadhaa ya hifadhi za jadi yanavuka mipaka, na hasa yale ya watu wa asili wanaohamahama.

[11]Hukumu muhimu ya Mahakama Kuu ya India hivi majuzi imehusu kutambuliwa kwa Ora huko Rajasthan.

[12] #Maeneo yaliyohifadhiwa. Tazama pia Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa – Kituo cha Ufuatiliaji wa Uhifadhi Duniani, 2016.

[13] Asatrizy and Riascos de la Peña, 2008.

[14] Mojawapo ya kanuni zilizobainishwa na E. Ostrom kama zinazohitajika kwa jamii za pamoja zinazofanya kazi vizuri. Tazama pia Robinson na wenzake., 2018; #Taasisi za Utawala.

[15] Bassi 2002; Bassi na Tache, 2011.

[16] Tazama ‘Tamko la Yaaballo kuhusu Mazingira Yaliyohifadhiwa ya Borana’ na jaribio la kuanzisha Hifadhi ya Jamii ya Mursi-Bodi http://coolground.org/?page_id=163.

[17] Hoole na Berkes, 2009; Borrini-Feyerabend na wenzake., 2010.

[18] Kutambulika humaanisha Eneo Lililohifadhiwa la Jamii (Aire du Patrimoine Communautaire) lililoanzishwa ndani ya maeneo yanayomilikiwa na umma kandokando ya mto.

[19] Cidrás na wenzake., 2018; Serrano na wenzake, 2018.

[20] John Stephen Okuta, alinukuliwa katika Borrini-Feyerabend na wenzake., 2010, ukurasa wa 55.

[21] Aman Singh, mawasiliano ya kibinafsi, 2019.