Usimamizi

Usimamizi na utawala – wakati zinaingiliana kwa karibu katika utendaji – zinaeleweka vyema shughuli tofauti. Usimamizi unahusu kutumia njia mahsusi na kutekeleza ili kufikia lengo fulani, yaani, “mchakato wa kukusanya na kutumia seti za rasilimali kwa njia iliyoelekezwa kwa lengo ili kukamilisha kazi katika shirika”.[1] Kwa mfano, eneo fulani linaweza kusimamiwa ili kuhakikisha utunzaji wa kazi zake za kiikolojia kupitia hatua mbalimbali: kupanga; kuandaa; bajeti na ugawaji rasilimali; kufanya shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria; matokeo ya ufuatiliaji; kutathmini na kurekebisha upya mipango kulingana na tunayo jifunza; n.k. Rasilimali zinazohitajika zinaweza kujumuisha rasilimali watu wenye uwezo husika, uzoefu na ujuzi; rasilimali fedha; aina mbalimbali za taarifa (kwa mfano, sheria, takwimu za ikolojia, masoko ya fedha); pamoja na maliasili (kwa mfano, ardhi, maji, mbegu, aina za wanyama na mimea, wachavushaji).

Katika muktadha wa michakato ambayo maeneo ya hzaifadhi  ya jadi ya Kongani hudumishwa na kuimarishwa na wamiliki wao, usimamizi kwa kawaida hujumuisha kuchora ramani ya eneo; kuweka mipaka yake na vipengele muhimu; kuelewa, kama kikundi, nini kinahitajika ili kufikia malengo yaliyoainishwa na jamii; kutekeleza kanuni za kufikia na kutumia zilizokubaliwa na jamii (inawezekana tayari imejumuishwa katika itifaki ya jamii; tazama #sheria za kimila na itifaki za jamii; #kwa njia inayofaa); kufanya ufuatiliaji au doria ili kupatikana heshima ya sheria; kuwazuia na kuwaadhibu wakiukaji; kupata mapato kwa ajili ya jamii ili kuendeleza ufuatiliaji na shughuli nyingine muhimu zinazoendelea; na kadhalika.

Ingawa jukumu la utawala wa jamii ni muhimu ili kuwa na eneo la hifadhi ya jadi la Kongani jukumu la usimamizi siyo. Kwa hivyo, ikiwa serikali ‘itakasimisha’ usimamizi wa eneo la hifadhi ya jadi kwa watu wa asili au jamii ya wenyeji, au kupendekeza mpango wa usimamizi wa pamoja kwao, hii kwa ujumla inakosa utambuzi wa kweli wa haki zao za kujitawala.

Baadhi ya wamiliki na jamii walichagua kutosimamia moja kwa moja maeneo yao na maliasili zinazopatikana humo. Hii inaweza kuwa kwa sababu za kitaalam (ukosefu wa teknolojia au vifaa), sababu za kisheria (mahitaji ya usalama) au sababu za kiutendaji (ukosefu wa wafanyakazi). Jukumu lao la ulinzi linatekelezwa kupitia utawala wao, huku utekelezaji wa maamuzi (usimamizi) ukikabidhiwa kwa wengine. [2]


Rejea muhimu:

Hitt, Black na Porter, 2011; Kothari na wenzake, 2015; Worboys na Trzyna, 2015.


[1] Hitt, Black na Porter, 2011, ukurasa wa 4.

[2] Kwa mfano, wanaweza kuwa siyo wao wanaokata au kuvuna miti, wanawaachia wataalamu walioajiriwa shughuli hizo, au wanaweza kutia saini makubaliano ya utunzaji wa ardhi na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayosimamia ufuatiliaji wa viumbe hai mbalimbali muhimu katika eneo lao.