
Wamiliki/Wasimamizi/Walezi
Watu wengi wa asili na jamii za wenyeji duniani kote hufanya kazi kama wamiliki, wasimamizi na walezi wa ardhi, maji, anga, udongo, madini, maliasili na bioanuwai wanazomiliki au kutumiwa kiutamaduni. Wazo la umiliki/usimamizi/ulezi [1] hujengwa juu ya mahusiano yao na maeneo yao, ambayo yanajumuisha desturi za kitamaduni, kiimani na kijamii zinazoelekezwa katika ulinzi wa majira ya asili, mifumo ikolojia, aina za viumbe hai na vipengele vya mandhari.
Kwa Mkataba Kuhusu Bioanuwai Tkarihwaié:ri Kanuni ya Maadili ya Kuhakikisha Kuheshimiwa kwa Urithi wa Kiutamaduni na Kiakili za Jamii za wamiliki wa Asili na Jamii za Wenyeji [2] zinatambua “muunganiko wa jumla wa ubinadamu na mifumo ikolojia na wajibu na majukumu ya jamii za asili na jamii, kuhifadhi na kudumisha jukumu lao la kitamaduni kama wamiliki wa jadi na wamiliki wa mifumo ikolojia hiyo kupitia kudumisha tamaduni zao, imani za kiroho na desturi za kimila”.
Jukumu la ulinzi la watu wa asili na jumuia za wenyeji kimsingi ni tofauti na utaratibu ambapo mamlaka huteua maeneo rasmi ya ‘kuhifadhiwa’ yanayozuia kutumia maliasili kwa njia za udhibiti kisheria pekee.
Kutenda kama mmiliki humaanisha “kuhifadhi mazingira kwa hiari, huku ukiishi nayo na kutokana nayo, na kuiweka kama amana kwa vizazi vijavyo.[3] Kwa njia nyingi kuwa mmiliki wa eneo ni sawa na kutawala – moja kwa moja ikiwa sio pia kisheria – kwa muda mrefu, kwa hisia ya uwajibikaji na kujali.
Umiliki wa jamii za asili au wenyeji unaweza kujumuisha kutumia sheria za nchi na vyombo vya sheria, na mamlaka za serikali zinazoweza kuingia ubia na watu wa asili na jamii za wenyeji. Jukumu la mmiliki kwa ujumla linaendana na muktadha, na linahitaji kueleweka kwa muktadha pia.
Jukumu la umiliki la watu wa asili na jamii za wenyeji linatambuliwa na mataifa katika ngazi ya kimataifa. Azimio la Rio la 1992 lilikubali kwa mara ya kwanza jukumu maalum na muhimu la jamii katika usimamizi na maendeleo ya mazingira, shukrani kwa ujuzi wao na desturi za kimila’. Tangu wakati huo, sheria ya kimataifa imezidi kutambua haja ya kusaidia juhudi za umiliki wa jamii. Utambuzi huu unajenga ufahamu kwamba, ili kudumisha jukumu kama hilo, watu wa asili na jamii za wenyeji wanahitaji kutumia uwezo na haki zao zinazohusiana na maarifa, desturi na maliasili.
Kuwatambua wamiliki wa maeneo ya hifadhi ya jadi ya Kongani
Ili eneo lifuzu kuwa eneo la hifadhi ya jadi la Kongani—ni muhimu kwamba watu wa asili au jamii ya wenyeji iwe kama mmiliki wa ardhi yake, maji, bioanuwai na zawadi nyingine zinazotokana na mazingira. Jukumu la umiliki la watu wa asili na jumuia za wenyeji ni muhimu ili kulinda na kuendeleza maeneo ya hifadhi ya jadi ambayo yamekamilika vyema na kutafuta kuboresha hali ya yale ambayo imevurugika au inayotazamiwa.
Huenda ikawa kwamba watu au jamii haiwezi tena, au bado haiwezi kutimiza nia yake ya kutunza eneo. Ile nia na kujitoa kufanya kazi kama wamiliki, hata hivyo, inaweza kuathiriwa na hali ambazo ziko nje ya uwezo wa jamii au watu. Mifano ya hali hizo zenye matatizo ni pamoja na mambo ya uchafuzi au wawindaji haramu kutoka nje ya eneo hadi migogoro na mawakala wa serikali au binafsi ambayo inazuia taasisi za utawala za jamii kutekeleza na kutumia kanuni zake (angalia #taasisi za Utawala).
Ikiwa hali ni hii, utambuzi fulani wa kisheria, au hata kutambuliwa kwa jamii na Serikali, jamii jirani, jamii za kiraia, na/au mashirika ya kimataifa yenye jukumu na mamlaka ya kujiamulia yanaweza kutoa usaidizi muhimu (tazama #Utambuzi Unaofaa). Kwa ujumla, #usalama wa umiliki wa pamoja wa ardhi, maji na maliasili ni njia yenye nguvu ya kuhimiza, kulinda, kuunda upya na kuongeza uwezo wa pamoja, utashi na jukumu la kujichukulia kama mmiliki wa eneo la hifadhi ya jadi la Kongani
Udini, imani kuu na uhifadhi
Zaidi ya asilimia 80 ya watu duniani wanajitambulisha kuwa wana imani za kidini/kiroho.[4] Imani nyingi duniani zinakubaliana na wazo hilo, linalotolewa kwa njia tofauti lakini zinazoendana, kwamba wanadamu wana wajibu wa ulinzi na majukumu ya pamoja kwa mazingira. Hii inaweza kuwa kwa sababu mazingira yanachukuliwa kuwa zawadi ya kimungu, au kwa sababu ni mwili hasa wa mungu/miungu au roho.
Imani za kiroho za wenyeji mara nyingi huelezewa vyema kuwa za asili kuliko za kawaida, au kama “aina za watu wa dini ya kawaida”.[5] Wengi wao wamekuza na kusambaza maarifa ya mazingira ya kitamaduni, matendo na desturi—kama vile heshima kubwa kwa maeneo mahususi na ‘maeneo matakatifu’, au marufuku ya kuharibu au kula aina mbali mbali ya viumbe fulani—ambazo huendeleza maisha endelevu na kustawisha hali ya kuwa mali ya eneo.
Imani kadhaa kuu (kama vile Ukristo, Uislamu, Uhindu, au Ubudha) huwaita waumini wao kutimiza wajibu wao wa usimamizi/ulinzi na kuchangia kuwasaidia katika kutunza mazingira yao—ndani na nje ya nchi. Imani kuu, hata hivyo, zina ‘mikondo ya mawazo’ tofauti sana. Tunu za wasomi wa daraja la juu zinaweza zisibebwe na makasisi wa chini na waumini. Na majukumu ya umiliki/usimamizi yanaweza yasitafsiriwe kirahisi katika vitendo.[6]
Tangu 1986 Mkutano wa Maombi ya Amani wa Assisi ambapo viongozi wa dini zote kuu za dunia walitoa maoni yao juu ya umuhimu wa kulinda mazingira, kutambuliwa kwa jukumu la pamoja la imani kwa vitendo kwa mazingira umekuwa kukiongezeka. Kwa mfano, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Imani kwa ajili ya Dunia unalenga kuhamasisha uhifadhi unaozingatia imani na kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Muungano wa Dini kwa ajili ya Uhifadhi pia unaunga mkono mipango ya kimazingira ya jamii za kidini. Fursa za kusaidia maeneo ya hifadhi za jadi zinaonekana kuwepo katika mwingiliano kati ya mipango ya imani na mapambano ya watu wa asili (tazama, kwa mfano, Mpango wa Misitu ya Mvua wa Madhehebu ya Dini Mbalimbali, Kundi la mafundisho ya Imani la Vatikani la Kukuza Maendeleo ya Kibinadamu, Laudato Sí Encyclica ya 2014).
Rejea muhimu:
Borrini-Feyerabend na wenzake., 2010; Verschuuren na wenzake. (tafsiri), 2010; Mkataba kuhusu Bioanuwai, 2011; Ruiz na Vernooy, 2012; McLeod na Palmer, 2015; Frascaroli, 2016; Frascaroli na Fjeldsted, 2017.
Tazama pia: Papa Francis, 2015; na filamu fupi kuhusu Utamaduni, Imani ya kiroho na Uhifadhi kutoka kwa Kikosi Kazi cha Tume ya Sera ya Mazingira, Kiuchumi na Kijamii cha Jamuiya ya Uhifadhi wa Biolojia ya Umoja wa Uhifadhi wa Mazingira Kimataifa kuhusu Utamaduni, Utakatifu na Uhifadhi kwenye. https://vimeo.com/349593871
[1] Tunakubali kwamba watu na jamii mbalimbali hutumia istilahi tofauti si tu kwa maeneo yao ya jadi bali pia kwa ajili ya majukumu yao yanayohusiana na hayo maeneo (kwa mfano, ‘wamiliki’, ‘wasimamizi’, ‘walezi’ na wengine). Muungano wa Kongani la Kimataifa kihistoria umetumia neno ‘wamiliki’ na mara nyingi hulitumia hapa kwa urahisi. Katika miktadha mbalimbali, maneno mengine yanafaa zaidi na yanapaswa kutumiwa.
[2] Mkataba kuhusu Bioanuwai 2011b.
[3] Borrini-Feyerabend na wenzake, 2010.
[4] Verschuuren na wenzake, 2010, ukurasa wa 2.
[5] Tofauti kati ya imani kuu na za asili ni muhimu lakini pia ni tatizo, kwani imani nyingi kuu ni za asili katika maeneo na tamaduni fulani, kama vile Uzoroastrianism, Daoism, na Jainism (Verschuuren na wenzake., 2010, ukurasa wa 3).
[6] Frascaroli na Fjeldsted, 2017.