Kuwezesha majadiliano mashinani

Wataalam wawezeshaji wa ndani: Wataalam wa uwezeshaji wa ndani ni kundi la wanajamii ambao wana ujuzi na shauku kuhusu eneo la hifadhi la jadi na wako tayari kuwezesha na kuandika mchakato wa kujiimarisha. Kwa hakika, wao ni watu wa kujitolea wenye uwezo na wanaoheshimika ambao huakisi na kufahamu utofauti wa jamii yao, ikiwa ni pamoja na watu kutoka katika makundi tofauti ya umri, jinsia, taaluma, hali ya kijamii na asili ya kitamaduni, kama itakavyohitajika. 

Timu hii imejichagua yenyewe na haina mamlaka maalum juu ya eneo husika au mchakato wa kujiimarisha. Inapohudumia jamii, inahitaji kuidhinishwa na jamii. Tunapendekeza Timu ijumuishe angalau watu watatu, na ikiwezekana, watano hadi saba.

Uwezeshwaji wa nje? Baadhi ya jamii huiomba timu ya uwezeshaji ya eneo husika kuongoza na kuwezesha mchakato mzima. Wengine huwaalika wawezeshaji kutoka nje. Ikiwa mwongozo huu utatumiwa na msimamizi wa nje, tunapendekeza kwamba timu ya uwezeshaji ya ndani iombwe kujiunga, kuunga mkono na kuongoza inapowezekana.

Mijadala ya mashinani: Mijadala ya mashinani ndiyo ‘mbinu’ kuu katika michakato ya kujiimarisha, ikitoa fursa za kutafakari na kufanya uchambuzi ndani ya jamii. 

Majadiliano ya mashinani hufanyika kwa njia zinazolingana na maisha ya kila siku. Hazina muundo maalum, kwani kila jamii hukutana kwa njia zinazofahamika na zinazolingana na muktadha wake. Kwa mfano, zinaweza kufanywa wakati wa mkutano mkuu wa kimila, kwenye baraza la wazee, au kwenye mikutano ya vikundi vya wanawake, umoja wa wakulima au vyama vya vijana.

Ikiwa kikundi kinachofanya majadiliano hakiakisi utofauti kamili wa jamii (k.m. kulingana na umri, jinsia, kabila, hali ya kijamii, n.k.) matokeo ya majadiliano yake yataunganishwa baadaye na mikutano zaidi. 

Majadiliano ya mashinani yanaweza kuanzishwa yenyewe, yakichochewa na tatizo au fursa mpya, au kuhimizwa na Timu ya Uwezeshaji. Kwa hakika, wanapata uwiano mzuri kati ya mazungumzo yanayompa nafasi kila mtu na yenye tija na yenye kuzingatia umakini.

Mijadala ya mashinani mara chache sana inatarajiwa kutoa uamuzi wa ndiyo/hapana. Badala yake, wanajadili somo kwa kina na – kwa kuwezeshwa na maswali – kubainisha faida na hasara za vitendo mbalimbali na kuchangia kuja na maamuzi mapya.

Mchakato: Kufuatia desturi au mila zinazofaa, Timu ya Uwezeshaji itaitisha mkutano wa awali ili jamii ijifunze kuhusu kujiimarisha na kuamua kama itaanzisha mchakato huo. Iwapo jamii itaamua kwamba, ndiyo, inataka kujiimarisha kama mmiliki wa eneo lao, Timu inatoa wito kwa mijadala kadhaa ya mashinani, itawezesha hayo na kuweka mkakati wa kufuatilia matokeo yake

Kila mjadala wa mashinani huzingatia kipengele tofauti cha mchakato na Timu huwezesha kwa kuuliza maswali muhimu kama sehemu ya kuanzia na mfumo wa marejeo

Mwongozo huu wa mtandaoni na Mwongozo wa kina zaidi (unaopatikana kama pdf) upo ili kusaidia Timu na kutoa mawazo kwa maswali na zana/nyenzo za kusaidia mikutano. Maswali hufanya mjadala kuwa makini na kuzuia kuzidiwa nguvu na watu wenye sauti zaidi, maslahi na maoni

Timu inaandika muhtasari wa matokeo, ikiwa ni pamoja na hitimisho kuu na mantiki ya washiriki tofauti, na vile vile kama kulikuwa na maoni yenye upinzani mkali. Ikiwa inafaa, Timu inaweza pia kupiga picha au video. Washiriki katika majadiliano mara nyingi wanakumbushwa kwamba jamii nzima ndiyo inayosimamia mchakato huo na inaweza kuchagua kwa uhuru cha kufanya na taarifa ambazo Timu inakusanya na kuziweka pamoja. Jamii pia ina jukumu la kuchambua, kutafsiri na kutumia matokeo ya majadiliano na kumbukumbu kuhusu eneo lao ambalo linatarajiwa kuimarishwa.

Muda: Hakuna muda uliowekwa wa mchakato wa kujiimarisha. Inaweza kuchukua siku, wiki, miezi, au hata miaka kutegemeana na kile ambacho jamii ingependa kufanya na wakati ambapo wanaweza na wangependa kutenga muda kwa ajili hiyo. Timu ya uwezeshaji inapaswa kupanga mchakato na jamii kama sehemu ya hatua za awali, kwa kuelewa kwamba mipango inaweza kubadilika.

Mambo ya kuzingatia kwa uwezeshaji wa kimaadili na ufanisi:

 • Kuheshimu tamaduni za wenyeji, itifaki na mila.
 • Hakikisha heshima na hali ya uwazi
 • Kuwa muwazi kuhusu faida na hatari zinazoweza kutokea kwa kujihusisha katika mchakato wowote. 
 • Kuwa thabiti, mwaminifu na muwazi.
 • Hakikisha kwamba washiriki wanaweza kujieleza katika lugha na istilahi zao wenyewe. 
 • Tambua mawazo na uwezo wa washiriki.
 • Kuwa msikivu hai na makini.
 • Kuwa na heshima, hisia na mvumilivu.
 • Jenga maelewano chanya na washiriki, mwenye kukuza uaminifu na kujiamini. 
 • Hakikisha kwamba washiriki wanazingatia malengo ya jumla katika akili zao.
 • Saidia kuelekeza mjadala kwenye kipengele cha mchakato kilicho hatarini.
 • Kuwa na ufahamu wa tabia na viwango vya ushiriki.
 • Chukua jukumu la kuwa msaada, la kuwa nao.
 • Wezesha mikutano tofauti kwa watu au vikundi maalum kila inapofaa au inapohitajika.
 • Iwapo kuna kutoelewana kuwa mtulivu na asiyeegemee upande wowote, saidia kufafanua masuala na kuyaleta kwenye maadili na malengo yoyote yaliyopo.
 • Vunjavunja masuala yanayokinzana katika vipengele ambavyo angalau makubaliano. yanaweza kupatikana. 
 • Weka kasi nzuri, ukizingatia maadili na makubaliano ya pamoja.