Uamuzi huru na wa hiari  

Kuweza kusema “ndiyo” au “hapana” kwa hatua au pendekezo lolote ambalo litaathiri ardhi, maji, bioanuwai za kitamaduni au haki za jamii kwa kawaida hujumuishwa chini ya usemi ‘Uamuzi huru na wa hiari’. Iwapo ‘Uamuzi huru na wa hiari ‘ utahakikishwa, jamii inaweza kufanya maamuzi bila shuruti, vitisho, au udanganyifu; kabla ya hatua yoyote inayotarajia uamuzi; na kwa kuzingatia taarifa zote muhimu kuhusu machaguo mbalimbali yanayopatikana, katika lugha na maumbizo zinazoweza kufikiwa. Michakato ya kufanya maamuzi inapaswa kuamuliwa na jamii na kutoa muda wa kutosha kufikia makubaliano mapana. Na jamii zinapaswa kupata msaada wa kisheria na kitaalam ikiwa wataomba1.

Ingawa ni lazima ‘Uamuzi huru na wa hiari’ uwepo kabla ya shughuli zozote kuanza, haipaswi kuwa tukio la ‘mara moja’ au suala la kuweka alama kwenye kisanduku. Ridhaa inapaswa kudumishwa kwa muda, ikijumuisha kuwa na michakato ya kuingia au kufuatilia kwamba makubaliano yanatekelezwa kama yalivyotarajiwa, na kwamba jamii inaweza kuibua wasiwasi au malalamiko mapya ikiwa matukio yasiyotarajiwa yatatokea.

‘Uamuzi huru na wa hiari’ ni kipengele muhimu cha kujitawala na haki ya pamoja ya watu wa asili inayotambuliwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Asili na vyombo vingine vya kisheria vya kimataifa. Pia ni mbinu bora ya kimaadili inayokubaliwa kwa upana kuhusiana na jamii zisizo za asili. Kwa bahati mbaya, kiwango cha ‘Uamuzi huru na wa hiari’ hauheshimiwi katika utendaji. Sheria na sera za kimataifa mara nyingi hutumia mashauriano na kuchukuliana ambayo hayafikii ridhaa halisi. Kwa maneno mengine, ridhaa inachukuliwa kama lengo la matarajio badala ya sharti la uingiliaji kati ulioidhinishwa na serikali kwenye maeneo asilia.

Hili lisiwazuie jamii kuomba ‘Uamuzi huru na wa hiari’ na kujitahidi iheshimiwe, ikiwezekana kwa msaada wa wengine!(tazama Mwongozo wa Kujiimarisha ‘Chukua hatua ukiwa na wengine’)


Rejea muhimu:

Hill, Lillywhite na Simon, 2010.


[1] Tazama Hill, Lillywhite na Simon, 2010.

  1. Tazama Hill, Lillywhite na Simon, 2010. ↩︎